New Updates

Kanuni za kukabiliana na Machafuko*

 

Kanuni za kukabiliana na Machafuko* 

Na kalam ya Iman the story teller presents 


Tumia sheria hizi 12 kutoka kwa Jordan Peterson zitakazokusaidia kukabiliana na machafuko sehemu zozote iwe kazini ama popote. Maana maisha ni mwendelezo wa mambo mawili ambayo ni machafuko na utulivu.


Machafuko au vurugu ni pale vitu vinavyokwenda tofauti na tulivyopanga, tofauti na mategemeo yetu. Na Utulivu ni pale vitu vinavyokwenda kama ambavyo tumepanga, vile ambavyo unategemea viende.


 Sheria hizo ni 👇👇

⚖️ 1.Simama wima mabega nyuma unapofanya mambo yako /kuwa mwenye kujiamini na mwenye muonekano bora.

⚖️2.Jichukulie kama mtu ambaye una wajibu wa kumsaidia./Usijiipuuze Jijali na jipende.

⚖️3.Jenga urafiki na watu wanaotaka uwe bora/si kila mtu awe rafiki yako.

⚖️4.Jilinganishe na wewe wa Jana na si mtu mwingine.

⚖️5.Usiruhusu watoto /watu wengine wafanye kitu kitakachokufanya uwachukie.

⚖️6.Tengeneza kwanza nyumba yako/Biashara yako kabla ya kuikosoa Dunia.

⚖️7.Fanya kile chenye maana kwako na si kilicho rahisi kufanywa na wewe.

⚖️8.Sema ukweli au Angalau usidanganye.

 ⚖️9.Chukulia kwamba mtu unayeongea naye ana kitu cha maana usichokifahamu. 

⚖️10.Kuwa makini kwenye kauli zako/sema kwa njia inayoeleweka.

⚖️11.Usiogope kufanya jambo la hatari kwa malengo ya kujijenga kuwa imara. Maana maisha yanataka watu imara.

⚖️12.Vifanye vitu vidogo vidogo kwa ubora na usivipuuze vipe mkazo kwakua makubwa hutokea kwenye udogo.

Timiza wajibu wako nao wajibu uliotimizwa utatimiza mahitaji yako. Wewe ni mshindi usiishi kama mshindwaji.

Tafiti zinaonyesha kwamba Strees/mawazo  hukaa akilini kwa mda wa dakika 20 baada ya apo wewe ndo utaamua  yaendelee kubaki au utaamua kuachana nayo.

Usiruhusu akili yako ibebe nyakati mbaya kila wakati, jaribu kupambana nayo kuondoa hiyo hali. 

No comments