GOD DOESN'T GIVE THE PEOPLE YOU WANT, HE GIVES THE PEOPLE YOU NEED.
𝗦𝗢𝗠𝗔 𝗛𝗜𝗜 𝗡𝗔 𝗨𝗝𝗜𝗙𝗨𝗡𝗭𝗘 𝗞𝗜𝗧𝗨
Binti mmoja alikua amekaa kibarazani analia, simu yake bado alikua ameishikilia mkononi anatetemeka. Alitokea Bibi mmoja ambaye hata hawakua wakifahamiana, yule Bibi alikaa pembeni yake na kumuuliza ni kwanini binti mzuri...✍️👇
kama yule alikua analia mchana wote ule. Huku akiendelea kulia, binti alianza kumlaumu Mungu, akisema haamini kweli kama Mungu yupo.
Alisema yeye anamuomba Mungu kila siku, anatoa sadaka, anasaidia masikini na anafunga lakini Mungu amemdanganya kwa muda mrefu na sasa kamuacha analia.
Bibi alimuuliza ni nini kimetokea lakini binti aliendelea kulia huku akilalamika akisema, mimi nimempa Mungu maisha yangu yote lakini ameshindwa kunipa kitu kimoja tu nilichokua namuomba kila siku. Bibi alimuuliza kitu gani binti akamuambia ndoa.
Alimuambia mpenzi wangu wa miaka saba ameniacha na kumuoa rafiki yangu kipenzi, niliwafumania na kumuomba msamaha lakini pamoja na mimi kutokukosea amenitumia meseji kuwa hanitaki na sasa anamuoa rafiki yangu,
kweli Mungu yupo? Kweli ananipenda? Angekua ananipenda angenifanyia yote haya, angeniumiza hivi?
Bibi alimuangalia na kutabasamu, kisha akamuambia Mungu anakupenda na ndiyo maana aliruhusu umfumania rafiki yako na mpenzi wako kabla ya kukuoa! Asingekua anakupenda asingekufungua macho.
Binti alikasirika na kuanza kutukana tena akidhani Mungu hampendi. Yule Bibi alimsogelea akamshika macho kisha yule Binti alilala palepale na kupata usingizi mzito, akiwa amelala Binti alianza kuota
Aliota harusi kubwa ya yeye na mpenzi wake, watu wengi wamehudhuria na kila mtu anafuraha, rafiki zake wote wapo hata yule aliyemfumania yupo na anafurahia ndoa yao.
Baada ya harusi alipata ujauzito, yeye na mume wake walikua wanaishi ndoa ya raha sana, alichukua mkopo Ofisini kwao na kumalizia kujenga nyumba yao, baada ya kumaliza tu kujenga alishangaa ghafla mume wake kabadilika, hampendi tena na hamhudumii kwa chochote.
Siku moja akiwa ametoka kazini na mimba yake, alimfumania mumewe akiwa na yule rafiki yake katika nyumba aliyojenga na mume wake, tena katika chumba kilekile anacholala na mumewe. Alipoongea mume wake alimpiga sana wakimchangia pamoja na rafiki yake, baada ya hapo akawa amepoteza fahamu waliondoka na kumuacha. Asubuhi alizinduka na kupata msaada kutoka kwa majirani ambao walimsaidia kumpeleka Hospitalini, mimba ilitoka.
Kwa bahati mbaya wakati anasafishwa alitolewa kizazi na kuambiwa hatapata mtoto tena, alirudi nyumbani akiwa hana matumaini ya kuishi na mumewe liporejea na kusikia tena zile taarifa alimuacha akimuambia hawezi kukaa na mwanamke ambaye hazai.
Palepale alistuka huku akitetemeka, hakumuona yule Bibi lakini alikuta kiratasi kilichokua pembeni yake, alikifungua na kukisoma, kilikua kimeandikwa.
“Unaona namna Mungu anavyokupenda, hakutaka upitie yote hayo ndiyo maana akakufungua macho sasa. Usiachae kumuombe kwani yeye hatendi kama tunavyotaka sisi bali hutenda kwa namna yake”.
Binti alijikuta analia, sasa hivi hayakua machozi ya huzuni bali machozi ya shukurani kwani Mungu alikua amemuepushia mambo mengi. Siku iliyofuata alienda kutoa sadaka nyingine na kumshukuru Mungu kwa wema wake.
************𝗠𝗪𝗜𝗦𝗛𝗢***************
Mungu anatenda, inaweza kuwa si kama tunavyotaka sisi lakini kama una imani hatakuacha uangamie kwa kuwa ana nguvu za ajabu.
𝗙𝗨𝗡𝗭𝗢
Tumtegemee Mungu katika kila jambo, kwa maana yeye anatupenda na anajua ni kitu gani bora kwetu.

No comments