New Updates

CODE MUHIMU KWA KINA DADA ITAKUSAIDIA KULA CHUMA IKO 👇👇 DADA HII NIMEKUIBIA SIRI MUHIMU NA IKUSAIDIE KABISA KATIKA MAHUSIANO YAKO Dada angu hii ikupe taswira na ujue unadate na mwanaume wa aina gani na ujifanyie tathimini ila kisha uone lipi njema. Mwanaume mwenye upendo na anayekuhitaji kabisa katika maisha yake ana sifa hizi👇👇

 


CODE MUHIMU KWA KINA DADA ITAKUSAIDIA KULA CHUMA IKO 👇👇

DADA HII NIMEKUIBIA SIRI MUHIMU NA IKUSAIDIE KABISA KATIKA MAHUSIANO YAKO


Dada angu hii ikupe taswira na ujue unadate na mwanaume wa aina gani na ujifanyie tathimini ila kisha uone lipi njema.

Mwanaume mwenye upendo na anayekuhitaji kabisa katika maisha yake ana sifa hizi

1. Ukimtembelea mwanaume au akikuambia njoo nimekumiss/tuongee lakini baada ya mdinyo hakuna lolote la maana la kuongea. Akiondoka kitandani akawa busy na mambo yake mara aondoke akuache pekee aende kwa marafiki zake (huyo hana lolote). Mwanaume mwenye ndoto na wewe hitaji lake haliishii kwenye mwili wako tu.

2. Ukiona mwanaume wako hataki ufike kwake ila yeye aje kwako au yuko radhi kulipia hotel mkae hata siku tatu ila kwake hapana piga chini hakuna mtu hapo.

3. Mwanaume kabla ya kukupata (kulala naye) alikuwa anakujali na kuonekana ni mtu ila mlipolala tu akaanza kuleta dharau fulanifulani na kuanza kuvunjia heshima weka pembeni usiogope kuhesabiwa idadi ya wanaume. Hitaji lako ni mume anayekupenda na kujithamini sio mtu mwenye uume.

5. Mwanaume anayelalamika na kukutia  hofu tu badala ya kukuaminisha kuhusu kesho njema hafai kuwa mume wala baba wa familia.

6. Mwanaume anayekudhihaki au kutaka kukudhoofisha baada ya kukupata, mwenye kauli za kejeli na dhihaka juu ya ndugu, maisha yako, kazi yako nk weka kwenye jalala.

7. Mwanaume lazima awe na kitu chochote kinachomwingizia kipato hata kidogo. Usidate na mtu ambaye hajui kupambana hata kubeba mizigo sokoni. Kumbuka huyo ni mume na baba wa familia ana wajibu wake katika ndoa yenu. Ukiona mtu wa aina hiyo mshauri kuhusu kufanya kazi.


8. Tabia za ndani na nje, mkiwa naye ndani au wawili anajibehavije upata taswira. Tabia za nje ni zako na jamii. Anaonekanaje, anahusianaje na watu na hulka zake. Tabia za nje (kwenye jamii) ni moja ya kitu muhimu sana kukitazama.

Note:sio kila mwnaume anafaa kuwa baba wa watoto wako hakikisha unakuwa na mwanaume ambaye unaona anafaa kuwa Baba wa familia.

No comments