MGOGORO KATI YA ISRAELI NA PALESTINA NINI KIFANYIKE?
MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA.
NINI CHANZO CHAKE, NINI KINAENDELEA NA NI IPI SULUHU YA KUDUMU?
Makala hii itaangazia uhalisia wa mgogoro kwa uwazi bila upendeleo. Hivyo kama una mihemko ya itikadi za kidini na kiushabiki nakushauri USISOME.
~Eneo la Israel na Palestina ni jumla ya -2679 km²
~Idadi ya wapalestina ni 5,350,000. Huku waisrael wakiwa ni 9,174,520.
~Taifa la Israeli limepakana na nchi za Misri, Syria, Lebanon na Jordan.
~Lugha rasmi ni Kiebrania na kiarabu.
~Dini za Israeli
Uyahudi - 74%
Uislam - 17%
Ukristo - 2%<<
~Dini za Palestina.
Uislam 97%
Ukristo 3%
HISTORIA YA ENEO LA MGOGORO HADI LEO.
Wakazi wa kwanza wa eneo hilo walikua ni Wayebusi, Waamori, Hahiti, Wakanaani, Waperizi nk.
Abraham ambaye ni Baba wa Uzao wa Waisrael alihama kutoka kwao Uru ya Wakaldayo (Iraq ya sasa) hadi eneo hilo mwaka 1900BC, ambapo aliishi na wenyeji kwa amani na kuzaa watoto wake hapo wakiwemo Ishmael na Isaka.
Isaka alimzaa Yakobo ambaye alibadilishwa jina na Kuitwa Israel
ambaye alizaa watoto 12 kabla ya kuhamia Misri yeye na uzao wake kuikimbia njaa iliyokumba eneo hilo.
Huko Misri walikaa miaka 400 na waligeuzwa watumwa na kupata mateso makali kabla ya Mungu kuingilia kati na kuwaokoa kwa kumtumia Musa.
Musa aliwaongoza Waisrael kutoka Misri kabla ya Yoshua kuchukua kijiti na kwenda kuliteka eneo la Kanaani. Hawakufanikiwa kuteka eneo lote waliloahidiwa na Mungu kwa sababu ya kutofuata maagizo yake.
Lakini ilipofika kipindi cha utawala wa Mfalme Daudi Ufalme wa Israel ulihimarika vizuri na kuteka eneo lote na kulikalia. Baada ya Daudi alitawala Sulemani kabla ya kumuachia utawala mtoto wake Rehoboamu ambapo Ufalme wa Israel uligawanyika mara 2.
Kulizaliwa Ufalme wa Yuda na Ufalme wa Israel ambapo falme hizo hazikudumu sana kwani zilianguka chini ya madola makubwa duniani.
Kwa kipindi cha miaka kama 1360 eneo hilo lilitawaliwa na Falme za Assyrian Empire, Babylonian, Persian, Greece, na Roman Empire. Hali hii ilisababisha Wayahudi wengi kutekwa na kupelekwa utumwani katika nchi mbalimbali duniani.
Waliacha jamii zingine zikiendelea kuishi hapo na katika mji wa Yerusalemu na mwaka 638AD eneo hilo liliangukia chini ya Dola ya Kiislam ya Rashidun Caliphate. Chini ya kiongozi Omar Al Khatwab ambaye alikabidhiwa funguo za Jiji la Yerusalemu na Kasisi wa Kirumi Sophronius kwa mkataba wa makubaliano kuhusu eneo hilo.
Mkataba wa makabidhiano ulifanyika katika kanisa la ‘Holy Sepulchre’ Mkataba huo kuhusu mji wa Yerusalemu uliitwa ‘OMAR TREAT’ na ulisomeka hivi;
Haya ndio ya amani anayowapa Umar kiongozi wa Waislam watu wa Yerusalemu. Amewapa amani kwa nafsi zao, makanisa yao na misalaba yao. Makanisa yao hayatakaliwa, kuvunjwa, kuongezwa wala kupunguzwa kitu katika majenzi wala nafasi yake. Hawatalazimishwa kuacha dini yao wala kudhuriwa na yoyote.
Katika kipindi hiko miji mingi ya eneo hilo la Israel waliingia waislamu wengi. Caliph Omar alijenga msikiti mdogo kwaajili ya Ibada ambapo Waislam wanaamini msikiti wa Al Aqsa uliotajwa kwenye Quran ulikuwa hapo.
Msikiti huo uliendelea kuongezwa ukubwa hadi kufikia muonekano wa leo. Ni eneo hilo ndipo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu kubwa kwaajili ya Mungu na Wayahudi wanaamini Hekalu la 3 na la mwisho litajengwa tena hapo.
Eneo lote hilo la Israeli lilikaa chini ya Utawala wa Rashidun kwa kipindi kisichopungua miaka 462. Kipindi hiki jamii nyingi za eneo hilo zilijifunza lugha ya Kiarabu na kubadili dini kwenda Uislam.
Mwaka 1095AD Utawala wa Rashidun uliangushwa na Dola ya Kirumi katika vita ya Msalaba ‘CRUSADE WAR’ Warumi walilikalia eneo hilo na Mwaka 1291 walifurushwa Utawala wa Mamluk.
Mwaka 1516AD eneo hilo liliangukia kwenye Dola ya Kiislam ya Ottoman. Dola ya Ottoman ilitawala eneo hilo hadi vita ya kwanza ya dunia iliposhindwa na eneo kuangukia katika mikono ya Waingereza.
MWANZO WA WAISRAELI KURUDI KWAO.
Kutokana na mateso, ubaguzi na manyanyaso waliyopata Waisrael waliamua kutafuta asili yao na mwishoni mwa karne ya 19 baadhi ya wayahudi waliona kuna umuhimu wa kuwa na taifa na utambulisho wao duniani ili waheshimiwe na kukimbia manyanyaso hayo.
Mwaka 1896 Mwandishi wa kiyahudi mzaliwa wa Austria Theodor Herzl alianza kupaza sauti kuhusiana na hilo. Aliandika Insha na kuandaa mkutano ambao uliamsha ari ya wayahudi kurudia ardhi yao ya asili.
Harakati zake zilisababisha waisrael kuhamia katika Ardhi ya Palestina. Mwanzo walikua ni waisraeli 20,000 lakini baada ya harakati zake waliongezeka hadi kufikia 160,000+
Mwaka 1917 kulianzishwa azimio lililojulikana kama ‘Balfour Declaration’ lilichochea harakati za Wayahudi kurudi nyumbani Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia na mauwaji ya Adolf Hitler dhidi ya wayahudi yalizidi kuamsha ari hiyo na baada ya vita ya pili ya Dunia Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza aliandika barua kwa Lord Rothschild mkuu wa jumuiya ya wayahudi Uingereza.
Mwaka 1947 Uingereza ilipeleka azimio la kuanzishwa kwa taifa la Uyahudi na umoja wa mataifa ulikubali kwa sharti la eneo hilo kugawanywa kwa pande mbili yaani Palestina na Israeli baada kutokea vita kati yao.
Wayahudi walikubaliana na azimio hilo na 14/05/1948 walianzisha rasmi taifa lao. Jumuiya ya Waarabu walikataa azimio hilo na waliona mpango huo ni ukoloni wa ulaya ndani ya mashariki ya kati.
Wakati huo Wayahudi walikua ni 650,000 na Wapalestina 1,200,000. Wapalestina kwa kusaidiwa na nchi za Syria, Misri, Iraq na Jordan walitangaza vita dhidi ya Israeli mnamo 15 Mei 1948.
Tarehe 10/03/1949 vita vilimalizia kwa Israeli kushinda na kuteka ardhi kuwa zaidi toka kwa Palestina na kusababisha wakimbizi zaidi ya 700,000. Na maelfu kuishi katika makambi ya ukimbizi hadi leo.
Kufikia leo zaidi ya wapalestina 9,000,000 ni wakimbizi duniani kote kutokana na mgogoro huo. Katika vita ya siku 6(six days of war) ambapo Israeli iliyachakaza vibaya mataifa ya kiarabu yaliyoungana dhidi yake, Israel ilijiongezea eneo lake kutoka Palestina kutoka 55% hadi 77%
Kutokana na mateso hayo wapalestina walianzisha vyama kama PLO na Hamas kwaajili ya kupambana na utawala wa kizayuni bila mafanikio.
SULUHU YA MGOGORO NI IPI?
Wachambuzi na wanadiplomasia walitoa mapendekezo mawili ya suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.
1. TAIFA MOJA.
Wazo hili linakubaliwa na waisrael walio wengi ila kwa sharti la kutowatambua wa palestina waliokimbia nje ya Israeli.
Kwa upande wao Palestina haikubaliani na wazo hili kwa hofu ya kwanza kupoteza utambulisho wao na pili kunyanyasika na kufanywa watu wa daraja la chini ndani ya nchi yao.
2. MATAIFA MAWILI.
Wazo hili linakubalika na pande zote mbili ila kikwazo ni Makaazi ya walowezi wa Kiyahudi ndani ya Ukingo wa Magharibi na hatma ya mji wa Yerusalemu.
Israeli inautambua Yerusalemu kama mji mkuu wake na tayari baadhi ya mataifa kama Marekani, Honduras, Guatemala na Kosovo yamehamisha Balozi zao kutoka Tel Aviv kwenda Yerusalemu.
Kitendo hicho kinalaaniwa vikali na Palestina kwa kuwa inauona huo mji kama ni mji mkuu wake wa Taifa lao lijalo.
Mji wa Yerusalemu ni mji muhimu sana kwa Dini kubwa 3 duniani za Ukristo, Uislam na Uyahudi na una maeneo mengi ya kihistoria ya dini hizo.
Na pande zote mbili hazitaki kuuachia huo mji.
Wewe unadhani suluhu ya kudumu ni ipi? Nani mchokozi na nani hana haki ya kuishi hapo?
Nasubiri maoni yako hapo chini bila matusi.
Credited by iman the story teller




No comments